OONI Measurement Aggregation Toolkit (MAT)

Tengeneza takwimu kuhusiana na jumla ya watu walioangalia data za OONI kwa wakati huohuo duniani kote
Msaada

MAT ni nini?

Zana ya Kujumlisha Vipimo ya OONI (MAT) ni zana inayokuwezesha kuunda chati zako maalum kulingana na jumla ya mionekano ya data ya wakati halisi ya OONI iliyokusanywa kutoka kote ulimwenguni.

Data ya OONI inajumuisha vipimo vya mtandao vilivyokusanywa na watumiaji wa OONI Probe kote ulimwenguni

Vipimo hivi vina maelezo kuhusu aina mbalimbali za udhibiti wa mtandao, kama vile kuzuia tovuti na programu duniani kote.

MAT ni ya nani?

MAT iliundwa kwa ajili ya watafiti, waandishi wa habari, na watetezi wa haki za binadamu wanaopenda kuchunguza udhibiti wa mtandao duniani kote.

Kwa nini utumie MAT?

Wakati wa kuchunguza visa vya udhibiti wa mtandao, ni muhimu kuangalia vipimo vingi kwa wakati mmoja ("jumla") ili kujibu maswali muhimu kama yafuatayo:

Je, majaribio ya huduma (k.m. Facebook) yanaonyesha dalili za kuzuiwa kila wakati inapojaribiwa katika nchi? Hii inaweza kusaidia kuondoa chanya zisizo za kweli.

  • Je, ni aina gani za tovuti (k.m. tovuti za haki za binadamu) zimezuiwa katika kila nchi?
  • Je, tovuti mahususi (k.m. bbc.com) imezuiwa katika nchi zipi? Je, uzuiaji wa huduma una tofautiana vipi katika nchi na ASNs?
  • Je, kuzuia huduma kunabadilikaje kwa wakati? Tunapojaribu kujibu maswali kama yaliyo hapo juu, kwa kawaida tunafanya uchanganuzi unaofaa wa data (badala ya kukagua vipimo kimoja baada ya kingine).

MAT inajumuisha mbinu zetu za uchanganuzi wa data, kukuwezesha kujibu maswali kama haya bila ujuzi wowote wa kuchanganua data, na kwa kubofya kitufe!

Jinsi ya kutumia MAT?

Kupitia vichujio mwanzoni mwa ukurasa, chagua vigezo unavyojali ili kupanga chati kulingana na maoni ya jumla ya data ya OONI.

MAT inajumuisha vichungi vifuatavyo:

  • Nchi: Chagua nchi kupitia menyu kunjuzi (chaguo la "Nchi Zote" litaonyesha mtandao wa kimataifa)
  • Jina la Jaribio: Chagua Jaribio la Uchunguzi wa OONI kulingana na ambalo ungependa kupata vipimo (kwa mfano, chagua Muunganisho wa Wavuti ili kuona jaribio la tovuti)
  • Kikoa: Charaza kikoa cha tovuti ambayo ungependa kupata vipimo (k.m. twitter.com)
  • Kategoria za tovuti: Chagua kategoria ya tovuti ambayo ungependa kupata vipimo (k.m. News Media kwa tovuti za ya habari)
    • ASN: Andika ASN ya mtandao ambayo ungependa kupata vipimo vyake (k.m. AS30722 kwa Vodafone Italia)
  • Kipindi cha tarehe: Chagua kipindi cha vipimo kwa kurekebisha vichujio vya Kutoka na Mpaka
  • Safu wima: Chagua thamani ambazo ungependa zionekane kwenye mhimili mlalo wa chati yako.
  • Safu mlalo: Chagua thamani ambazo ungependa zionekane kwenye mhimili wima wa chati yako.

Kulingana na kile ungependa kuchunguza, rekebisha vichujio vya MAT ipasavyo na ubofye Onyesha Chati.

Kwa mfano, ikiwa ungependa kuangalia majaribio ya BBC katika nchi zote duniani:

  • Andika www.bbc.com chini ya Domain
  • Chagua Nchi chini ya Safu mlalo
  • Bofya `Onyesha Chati

    Hii itapanga chati nyingi kulingana na majaribio ya OONI ya www.bbc.com duniani kote

    Kutafsiri chati za MAT

Chati za MAT (na jedwali zinazohusiana) ni pamoja na vipimo vifuatavyo:

  • OK count: Vipimo vilivyofaulu (yaani HAKUNA dalili ya udhibiti wa mtandao)
  • Idadi iliyothibitishwa: Vipimo kutoka kwa kiotomatiki tovuti zilizozuiwa zilizothibitishwa (k.m. ukurasa wa kuzuia ulitolewa)
  • Hesabu isiyo ya kawaida: Vipimo vilivyotoa ishara za uwezekano wa kuzuia (hata hivyo, false positives vinaweza kutokea )
  • Idadi ya kushindwa: Majaribio yasiyofaulu ambayo yanapaswa kutupwa
  • Idadi ya vipimo: Jumla ya ujazo wa vipimo vya OONI (zinazohusiana na nchi iliyochaguliwa, rasilimali, n.k.)

Unapojaribu kutambua kuzuiwa kwa huduma (k.m. twitter.com), ni muhimu kuangalia kama:

  • Vipimo vinafafanuliwa kama imethibitishwa, na kuthibitisha kiotomatiki kuzuiwa kwa tovuti
  • Kiasi kikubwa cha vipimo (ikilinganishwa na hesabu ya jumla ya kipimo) kinawasilisha mapungufu (yaani dalili za uwezekano wa udhibiti)

Unaweza kufikia data ghafi kwa kubofya pau za chati, na kisha kubofya viungo husika vya kipimo.

Aina za tovuti

OONI Probe users test a wide range of websites ambayo iko chini ya aina 30 zilizosanifiwa.

Pombe & dawa ya kulevya
Tovuti zinazohusiana na matumizi, vifaa na uuzwaji wa madawa ya kulevya na pombe kinyume na sheria za sehemu husika.
Vifaa vya kutojulikana na kukwepa udhibiti
Tovuti zinazotoa vifaa vinavyotumika kwa ajili ya kutojulikana mtandaoni, kukwepa udhibiti wa mtandao, huduma za Proxy na usimbaji.
Vifaa vya Mawasiliano
Tovuti na vifaa kwa ajili ya mawasiliano ya mtu binafsi na makundi. Ikijumuisha webmail, VoIP, ujumbe wa papo kwa papo, majadiliano kwa njia ya maandishi na programu za ujumbe mfupi za simu.
Dhibiti maudhui
Maudhui ya wema au kutokuwa na hatia yakitumika kama udhibiti.
Utamaduni
Maudhui yanayohusiana na burudani, historia, fasihi, muziki, filamu, vitabu, ucheshi na dhihaka.
Biashara ya kielektroniki
Tovuti za huduma na bidhaa za biashara.
Uchumi
Maudhui yahusianayo na maendeleo ya kiuchumi na hali ya umaskini, wakala na fursa za kupata ruzuku.
Mazingira
Uchafuzi wa mazingira, mikataba ya kimataifa ya mazingira, ukataji miti, haki za mazingira, majanga nk.
Sambaza faili
Tovuti na vifaa vinavyotumika kusambaza mafaili, ikijumuisha mafaili yanayohifadhiwa mtandaoni, torrents na vifaa P2P vya kusambazia mafaili.
Kamari
Tovuti za kamali za mitandaoni. Ikijumuisha michezo ya kasino, kamali za michezo nk
Michezo
Michezo ya mtandaoni na majukwaa ya michezo, isipokuwa michezo ya kamali.
Serikali
Tovuti zinazoendeshwa na serikali ikiwemo tovuti za jeshi.
Vifaa vya Utapeli
Tovuti zinazolenga usalama wa kompyuta, ikijumuisha habari na vifaa. Inajumuisha maudhui salama na yasiyo na usalama.
Hotuba ya Chuki
Maudhui ya kudharau kundi fulani au watu kwa kuzingatia rangi, jinsia, au sifa zingine
Majukwaa ya kutunza tovuti na Blogi
Huduma za usimamizi wa tovuti, blogi na majukwaa mengine ya uchapishaji mtandaoni.
Maswala ya Haki za Binadamu
Tovuti zinazolenga kujadili masuala ya haki za kibinadamu katika mifumo mbalimbali. Ikijumuisha haki za wanawake na haki za makundi ya watu wachache katika jamii.
Taasisi zinazoingiliana na Serikali
Tovuti za taasisi zinazoingiliana na serikali kama vile Umoja wa Mataifa.
LGBTQ+
Mfululizo masuala ya LGBTQI (bila kuhusisha mambo ya ngono)
Kusambaza vyombo vya habari
Majukwaa ya kusambaza maudhui ya sauti, au video.
Maudhui mtambuka
Tovuti zisizoingia katika kundi lolote (XXX vitu vya hapa vinatakiwa kuwa katika makundi)
Vyombo vya Habari
Kundi hili linahusisha vyombo vya habari vikubwa (BBC, CNN nk) pamoja na taasisi za habari za nchi na vyombo vya habari binafsi.
Mahusiano mtandaoni
Huduma za kutafuta mahusiano mtandaoni ambazo zinaweza kutumika kukutana na watu, kutuma wasifu, mawasiliano nk
Ukosoaji wa Kisiasa
Maudhui yanayolenga hoja za kisiasa. Ikijumuisha watunzi muhimu na watu wa blogi, pamoja na taasisi za pinzani za kisiasa. Ikijumuisha maudhui ya umuhimu wa demokrasia, kupinga rushwa, pamoja na maudhui yanayohamasisha mabadiliko katika uongozi, maswala ya utawala, mabadiliko ya sheria nk.
Picha za ngono
Picha na video za ngono.
Mavazi ya kuchochea
Tovuti zinazoonyesha mavazi ya uchochezi au kumpa mwanamke maudhui ya kingono,kwa kuvaa nusu uchi.
Afya ya Umma
Virusi vinavosababisha Ukimwi, Virusi katika mfumo wa upumiaji, mafua, vituo vya kudhibiti magonjwa, Shirika la afya Duniani nk
Dini
Tovuti zinazohusiana na mijadala ya dini, yote ya kukosoa na kukubaliana, pamoja na imani za watu wachache katika jamii.
Injini za Utafutaji
Programu za kuperuzi na tovuti zinazokuwezesha kupata tovuti zingine.
Elimu ya jinsia
Inajumuisha uzuiaji wa mimba, kujizuia kujamiiana, magonjwa ya zinaa, ngono salama, mimba za utotoni, kuzuia ubakaji, kutoa mimba, haki za kijinsia na huduma za afya ya uzazi.
Mitandao ya Kijamii
Vifaa na majukwaa ya mitandao ya kijamii
Ugaidi na Wanamgambo
Tovuti zinazo hamasisha ugaidi, ukatili wa jeshi au harakati za kujitenga.